MKOPO WA VYOMBO VYA MOTO
Mkopo huu unalenga kumuwezesha mkopaji kufanya Maendeleo binafsi kwa kununua chombo cha moto cha biashara kama Gari, Bajaji au Pikipiki.
- 1. Mkopaji atajaza fomu maalumu ya kuomba mkopo
- 2. Mkopaji atatoa mchanganuo wa vyombo vya moto na jumla ya bei kwa vyombo vya moto anavyotaka kununua.
- 3. Mkopaji ana hiari ya kuchagua muda wa Marejesho kuanzi miezi 6 hadi miezi 48.
- 4. Riba ya mkopo wa vyombo vya moto ni asilimia mbili 2%
- 5. Mkopaji anaweza kukopa mkopo ambao ni mara moja (1), mbili (2) au tatu (3) ya akiba alizojiwekea.
- 6. Mkopaji atahitajika kuwa na kiasi cha Hisa zinazowiana na viwango vilivyowekwa kwa viwango mbalimbali vya mikopo.
- 7. Dhamana ya mkopo huu ni pamoja na:
- a. Hisa, Akiba, Amana ya mwanachama
- b. Mradi wenyewe kupitia biashara akaunti
- c. Hati mbalimbali za mali zisizohamishika.
- 8. Dhamana itakuwa ndani ya Mkoa wa Mbeya
- 9. Kiwango cha juu cha mkopo huu kitakuwa ni Tshs.200, 000,000/=
- 10. Mwanachama anayeruhusiwa kukopa mkopo huu ni yule aliyejiunga zaidi ya mwaka mmoja ndani ya Ushirika huu.
- 11. Mkopaji atajaza mkataba wa mkopo na LULU SACCOS itampa chombo alichonunuliwa.