Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
MKOPO WA DHARURA

Mkopo huu unalenga kumsaidia mwanachama mkopaji anapokuwa amepata dharura ya kibiashara yake, mkopo wa dharura umegawanyika katika sehemu mbili

  • 1. DHARULA INAYOHUSU MAJANGA MBALIMBALI;
  • (i)Mwanachama anapokuwa amepata matatizo na anahitaji msaada haraka, mfano kifo, ajali na majanga mengine yatakayodhibitishwa na kamati ya mikopo, mkopo huu hautazidi shilingi 5,000,000/=na utarejeshwa kwa mwezi mmoja hadi minne. (ii)Riba ya mkopo huu ni 1%
  • 2. DHARULA INAYOHUSISHA BIASHARA
  • Mwanachama anapokuwa amepata dharura ya kibiashara mfano, fedha ya kukombolea mzigo na kuboresha biashara yake. Mkopo huu maelezo ya uhitaji wake yatadhibitishwa na kamati ya mikopo.Masharti yake ni pamoja na ;
  • a. Mwombaji atajaza fomu maalum ya mkopo wa dharula
  • b. Marejesho ya mkopo huu ni mwezi mmoja au miwili
  • c. Riba ya mkopo huu ni 2% kwa mwezi.
  • d. Kiwango cha juu cha mkopo huu kitakuwa shilingi 200,000,000/= na itategemea dhamana pamoja na biashara ya mwombaji.
  • e. Mwanachama ataruhusiwa kukopa mkopo huu endapo amerejesha nusu ya mkopo wake wa biashara.(vinginevyo kuwe na nyaraka maalum zinazoonyesha umuhimu wa kupewa mkopo huu)
  • f. Mkopo huu hautatolewa kwa kujirudiarudia kila mwezi isipokuwa kama kuna sababu maalumu.
  • g. Mkopaji atajaza mkataba wa mkopo.
  • h. Mwanachama atapata mkopo huu bila kuweka mafungu ya Hisa na Akiba kwani mkopo huu ni huduma kwa Wanachama.
News 1
Karibu Sana

Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

picture-ya-Pesa
Vyanzo vya Mapato

  • (a) Hisa za wanachama
  • (b) Malimbikizo ya faida
  • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
  • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
  • (e) Akiba za wanachama
  • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

Ufahamu Zaidi

BIMA YA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
USIMAMISHAJI MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
UREJESHAJI WA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More