Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
MUUNDO WA CHAMA

  • Utangulizi
  • Muundo wa chama unajumuisha Mkutano Mkuu, Bodi ya Chama, Kamati mbali mbali, Meneja, Idara na vitengo vyake kama ilivyo katika sera ya utumishi. Pamoja na hayo, kwa kipindi cha miaka mitano chama kinaweza kuboresha muundo wake hivyo kupelekea kuongeza watendaji ili kutekeleza mikakati ya Chama kwa wakati.
  • Mkutano Mkuu
  • Hiki ndicho chombo kikuu cha maamuzi katika Chama.
  • Bodi ya Chama
  • Hiki ndicho chombo kikuu cha usimamizi wa shughuli zote za chama ambacho huchaguliwa na wanachama katika mkutano mkuu wa chama.
  • Kamati ya Usimamizi
  • Kamati hii itakuwa na wajumbe watatu ambao wamechaguliwa na Wanachama kwa ajili ya kuhakikisha kuwa,taratibu za uendeshwaji wa chama unazingatia Sheria ya Vyama vya ushirika Na. 06 ya mwaka 2013 na Masharti ya chama pamoja na miongozo mingine.
  • Kamati ya Mikopo
  • Kamati hii itakuwa na wajumbe watatu ambao huchaguliwa miongoni mwa wajumbe Bodi. Kazi kuu ya kamati ya mikopo ni kusimamia utaratibu wa utoaji, ufuatiliaji na kuishauri Bodi juu ya utoaji na ufatiliaji wa mikopo mibaya kwa kuzingatia Sera ya Mikopo ya Chama.
  • Meneja
  • Huyu ni mtendaji ambaye ameajiriwa na Bodi ya chama kwa ajili ya kusimamia maswala ya kila siku ya chama.Moja ya kazi muhimu ya Meneja ni:-
  • 1. Kuandaa, kutekeleza na kusimamia sera na taratibu za chama.
  • 2. Kuaandaa taarifa zote za fedha za kila mwezi, kila Robo mwaka na kwa kila mwaka.
  • 3. Kazi nyinginezo kwa mujibu wa maelekezo ya Bodi ya chama na kanuni za utumishi za chama.
  • Mkaguzi wa Ndani
  • Mkaguzi wa ndani atakuwa na jukumu la kuhakikisha kuna uthibiti bora wa mifumo ya ndani pamoja na majukumu mengine kama yalivoainishwa katika kanuni ya 56 ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2019.
News 1
Karibu Sana

Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

picture-ya-Pesa
Vyanzo vya Mapato

  • (a) Hisa za wanachama
  • (b) Malimbikizo ya faida
  • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
  • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
  • (e) Akiba za wanachama
  • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

Ufahamu Zaidi

BIMA YA MIKOPO

Mkopo ni chachu ya maendeleo na husaidia...

Read More
DHAMANA YA MKOPO

Wadhamini wa mkopo watawajibika moja kwa moja...

Read More
UIDHINISHAJI WA MIKOPO

Uidhinishaji wa maombi ya mikopo.LULU SACCOS ha...

Read More