Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
BIMA YA MAISHA YA MIKOPO

Mkopo ni chachu ya maendeleo na husaidia sana katika kuboresha maisha yetu, kwani fedha zinazokopeshwa hutumika kwa shughuli mbalimbali za maendeleo binafsi. Lakini inapotokea mkopaji amefariki kabla ya kumaliza marejesho ya mkopo huwa anaiweka familia katika mzigo mkubwa wa deni na vile vile kumkosesha mkopeshaji mtaji wake anaoutumia kukopesha wanachama wengine.

Kwa kuzingatia hili chama kitaendeleza mpango wa kujiunga na bima ya maisha ya mikopo itakayomkinga mkopaji na mkopeshaji, ambapo mkopaji atatakiwa kulipia bima hiyo kabla ya kupewa mkopo.Kutakuwa na aina mbili za bima, (a)Bima ya Ndani Bima ya ndani itakusanywa na Lulu SACCOS kwa kufungua akaunti ya ukusanyaji wa malipo ya bima hiyo ndani ya chama, ambapo mkopaji akipata majanga chama kitawajibika kulipa deni lililobaki la mkopaji kwa kutumia akaunti hii.

(b)Bima ya Nje Bima ya nje italipwa na mkopaji kwa makampuni yaliyoingia mkataba na chama.

Jinsi Bima Inavyofanya Kazi

  • 1. Bima hukatwa na Mwanachama mwenye mkopo
  • 2. Bima hulipwa pale mwanachama anapofariki
  • 3. Iwapo kifo cha mwanachama kitatokea, bima italipa mkopo pamoja na gharama zake.
  • 4. Warithi wanapata uhakika wa kutimiza ndoto zao
  • 5. Kiwango cha deni alilobakiza kitalipwa na bima husika
  • 6. Wadhamini hawatakuwa na wasiwasi wa kulipa deni
  • 7. Bima itawaondolea Saccos usumbufu wa kuwafuatilia warithi wa aliyekopa ili walipe deni lililobakia

Iwapo mwanachama atapata ulemavu wa kudumu:-

  • Wadhamini hawatakuwa na wasiwasi wa kulipa deni
  • Bima italipa deni lililobakia Saccos pale ulemavu wa kudumu unapotokea.
  • Bima kwa mikopo ya vikundi
    • 1. Mikopo ya vikundi itakingwa na bima ya maisha ya mkopo
    • 2. Wanakikundi wataleta orodha yao na namna walivyokopeshana katika kikundi chao na kuwasilisha majina yao Lulu Saccos na Lulu Saccos itahusika kupeleka majina hayo kwenye kampuni ya bima yakiwa yameshakingwa na bima.
    • 3. Endapo mwanakikundi au Mwanachama yeyote atafariki au atafiwa na mume au mke, watapata mafao ya mazishi kwa kupokea rambirambi kulingana na utaratibu uliowekwa na LULU SACCOS kwa makubaliano maalum na kampuni ya bima husika.
    • 4. Mkopo uliobaki na uliondani ya kipindi cha mkataba utalipwa na bima mwanakikundi akifariki.
    • 5. Kikundi kitawasilisha vielelezo vya kifo cha mwanakikundi huyo katika ofisi za Saccos na Saccos itapeleka vielelezo hivyo katika ofisi ya bima.
    • 6. Saccos itaeleza ni kiasi gani anachodaiwa mwanakikundi huyo aliyefariki.
    News 1
    Karibu Sana

    Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

    picture-ya-Pesa
    Vyanzo vya Mapato

    • (a) Hisa za wanachama
    • (b) Malimbikizo ya faida
    • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
    • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
    • (e) Akiba za wanachama
    • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

    Ufahamu Zaidi

    BIMA YA MIKOPO

    Mkopo ni chachu ya maendeleo na husaidia...

    Read More
    DHAMANA YA MKOPO

    Mkopo ni chachu ya maendeleo na husaidia...

    Read More
    UIDHINISHAJI WA MIKOPO

    Uidhinishaji wa maombi ya mikopo.LULU SACCOS ha...

    Read More