Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
MASWALI NA MAJIBU (FAQ)

  • Ni utaratibu upi unatumika kujiunga na LULU SACCOS?
  • 1. Awe mfanyabiashara na biashara yake iwe katika mkoa wa Mbeya
  • 2. Awasilishe barua ya maombi.
  • 3. Alete barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa anakoishi.
  • 4. Alete wadhamini watatu ambao ni wanachama wa LULU Saccos
  • 5. Atatembelewa na na viongozi wa chama ili kujiridhisha na biashara anayofanya ambapo TIN number na leseni ya biashara vitakaguliwa
  • 6. Kujaza fomu ya uanachama.
  • 7. Kulipa ada ya kiingilio kiasi cha Tzs 1,000,000
  • 8. Kulipia HISA 200 zenye thamani ya Tzs 2,000,000
  • 9. Kulipia hisa 50 za jengo kila hisa 10,000/= jumla 500,000/=
  • 10. Kulipia sera ya chama pamoja na T-shirty mbili jumla 54,500/=
  • 11. Kulipia bima ya mfuko wa jamii jumla 100,000/=
  • 12. Jumla ya gharama za kujiounga ni Tzs.5,654,500/=
  • 13. Tuma risiti za malipo kwa barua pepe: lulusaccos@gmail.com
  • 14. Kuwasilisha fomu zilizojazwa kwa ukamilifu kwenye ofisi za Chama kwa email au kwa mkono.
  • 15. Ambatanisha picha mbili za passport size.
  • Je mtu akishajiunga na chama itachukua muda gani kupata mkopo?
  • Mwanachama mpya atapata stahiki ya kuomba mkopo mara baada ya kulipa kiingilio,kukamilisha kulipia hisa na akiba za lazima na awe amekaa si pungufu ya miezi mitatu tangu kujiunga.
  • Mwanachama akiomba mkopo, mkopo wake unachukua muda gani kukamilika na pesa kuwekwa kwenye Account?
  • 1. Mkopo wa dharura unachukua siku moja au mbili.
  • 2. Mikopo mingine yote utolewa mara mbili kwa mwezi yaani tarehe 15 na tarehe za mwisho wa mwezi kwa kila mwezi.
  • NB: Ikumbukwe kwamba Mwanachama ana wajibu kuhakikisha anakamilisha kujaza fomu na mkataba wa mkopo husika, mkataba kisha kuzirejesha ama kwa mfumo laini ama kwa kuzileta fomu halisi katika ofisi za chama kuwezesha mchakato wa kutoa mkopo huo.
  • Kiasi cha juu cha mkopo ni shilling ngapi? Na muda wa mwisho wa marejesho miaka mingapi?
  • 1. Mkopo wa elimu kiwango cha juu ni sh. 5,000,000 (Muda wa marejesho ni miezi 6).
  • 2. Mkopo wa Dharura kiwango cha juu ni 200,000,000/= muda wa marejesho miezi miwili.
  • 3. Mkopo wa Dharura kiwango cha juu ni 150,000,000/= muda wa marejesho ni miezi miwili.
  • 4. Mikopo mingine kiwango cha juu ni sh. 600,000,000 muda wa marejesho ni miezi 48
  • Je naweza kukopa hata bila kuwa na michango?
  • 1. Anayeruhusiwa kukopa ni Mwanachama hai
  • 2. Kwa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa pasipo kuangalia kiasi cha akiba alichonacho kwenye Chama.
  • 3. Mikopo mingine mwanachama atakopeshwa kiasi cha mkopo kisichozidi mara 2, 3 au mara 4 ya akiba zake.
  • Je naweza kupunguza /kuchukua sehemu ya akiba zangu kidogo badala ya kukopa?
  • 1. Hairuhusiwi kupunguza au kuchukua sehemu ya hakiba kama una mkopo.
  • 2. Akiba za lazima haziwezi kurejeshwa au kupunguzwa kwa Mwanachama isipokuwa tu uanachama unapokoma.
  • Ni utaratibu gani unaotumika kupata mkopo?
  • 1. Lazima kwanza muombaji wa mkopo awe Mwanachama hai wa LULU SACCOS.
  • 2. Kujaza kikamilifu fomu husika ya maombi ya mkopo.
  • 3. Kuwasilisha fomu ya maombi kwenye ofisi za Chama.
  • 4. Kutembelewa na kamati ya mikopo ili kukagua dhamana .
  • 5. Kamati ya mikopo kukaa na kujadili ombi la mkopo
  • 6. Kusaini mkataba wa mkopo baada ya kamati ya mikopo kuidhinisha mkopo huo.
  • 7. Kuandikiwa cheki na kupelekwa benki kwa ajili ya kuingiziwa fedha ya mkopo kwenye akaunti ya benki au akaunti ya amana.
  • Je naruhusiwa kupunguza Mkopo?
  • Ndiyo. Mwanachama anayetaka kupunguza DENI kwa kulipa sehemu ya mkopo alionao katika Chama, atatakiwa kuandika barua ya kusudio hilo kwa Mwenyekiti wa Chama na katika barua hiyo atataja kiasi ambacho anataka kulipa kisha ataruhusiwa kufanya hivyo na atapewa nambari ya akaunti ambayo atatakiwa kuingiza fedha hizo benki na kisha kuwasilisha Hati ya Malipo katika ofisi za Chama.
  • Je naweza kulipa mkopo wote kwa mkupuo na utaratibu ukoje?
  • Ndiyo.
  • 1. Mwanachama atatakiwa kuandika barua ya kusudio la kulipa kwa Mwenyekiti wa Chama.
  • 2. Mkuu wa idara ya mikopo au Afisa Mikopo atakokotoa kiasi cha deni lililosalia.
  • 3. Mwanachama ataruhusiwa kufanya hivyo na atapewa nambari ya akaunti ambayo atatakiwa kuingiza fedha hizo benki au katika akaunti yake ya amana.
  • 4. Mwanachama atalipa mkopo uliosalia bila riba yake (endapo mkopo umekuwa ukirejeshwa kama ilivyo kwenye jedwali la mkopo).
  • 5. Mwanachama atawasilisha Hati ya Malipo katika ofisi za Chama.
  • Kwa nini ninatakiwa kuwa na wadhamini wa mkopo wakati tayari chama kinakata bima kwenye mkopo wangu? Je Bima inatumika wapi?
  • 1. Kuwa na mdhamini wa mkopo ni hitaji la kisheria
  • 2. Kazi ya Bima ya Mkopo kwa mujibu wa Sera ya Mikopo ni Kinga dhidi ya bakaa ya Mikopo itakayokua imeachwa na wanachama waliofikwa na aidha mauti/kufariki au Mwanachama aliepatwa na ulemavu wa kudumu na kushindwa kufanya kazi.
  • 3. Pale mwanachama anaposhindwa kurejesha mkopo kwa sababu zingine tofauti na hizo za kipengele na. 2 juu, mdhamini anawajibika kusaidia kufanikisha marejesho ya mkopo huo.
News 1
Karibu Sana

Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

picture-ya-Pesa
Vyanzo vya Mapato

  • (a) Hisa za wanachama
  • (b) Malimbikizo ya faida
  • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
  • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
  • (e) Akiba za wanachama
  • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

Ufahamu Zaidi

BIMA YA MIKOPO

Mkopo ni chachu ya maendeleo na husaidia...

Read More
DHAMANA YA MKOPO

Wadhamini wa mkopo watawajibika moja kwa moja...

Read More
UIDHINISHAJI WA MIKOPO

Uidhinishaji wa maombi ya mikopo.LULU SACCOS ha...

Read More