MIKOPO YA WATUMISHI
Aina ya Mikopo ya Watumishi ni kama ifuatavyo:-
(a)
Mkopo wa maendeleo kwa Mtumishi
Mkopo wa maendeleo wa Watumishi utakopeshwa kwa Watumishi wenye ajira ya Mkataba na LULU SACCOS. Vigezo vifuatavyo vitatoa mwongozo wa utoaji wa Mikopo ya Watumishi.
- 1. Mikopo ya Watumishi itakopeshwa kwa watumishi wenye Ajira ya Mkataba wa LULU SACCOS.
- 2. Mtumishi mwenye Ajira ya ya mkataba anayeweza kukopeshwa Mkopo huu ni yule ambaye amemaliza miezi mitatu (3) au sita (6) ya uangalizi (Probation Period) baada ya kuajiriwa.
- 3. Dhamana ya Mikopo ya Watumishi itakuwa:-
- i-: Mali isiyohamishika ya Mkopaji mwenyewe.
- ii-: Mshahara wake na posho
- 4. Riba yake itakuwa asilimia 0.5%
- 5. Mkopo huu utakopeshwa kwa muda wa miezi sita hadi thelathini na sita (36) kwa Mtumishi aliyeajiriwa. Kwa ajira ya Mkataba atapewa muda wa marejesho unaolingana na muda uliosalia kwenye mkataba wa ajira yake.
- 6. Kiwango cha mkopo kitazingatia kiwango cha mshahara na posho kwa kuzingatia mahitaji na marejesho ya mkopo yatakatwa na kubaki na asilimia 20 ya mshahara na posho zake.
- 7. Mtumishi ataomba mkopo mwingine baada tu ya kukamilisha malipo ya mkopo wa awali, isipokuwa dharula kama salio la mshahara na posho ni zaidi ya 20%.
- 8. Marejesho ya mikopo ya Watumishi yatafanyika kwa kukatwa kutoka kwenye mshahara na posho kila mwezi bila kukosa hadi pale deni lote litakapomalizika kulipwa.
- 9. Mikopo itaombewa kupitia fomu maalum za Mikopo ya Watumishi. Fomu zote zitaidhinishwa na Meneja wa Chama kabla ya kupelekwa kwenye kamati za mikopo na Bodi ndio itakayojadili na kupitisha mikopo ya Watumishi.
- 10.Mkopo wa Watumishi utazingatia kiasi cha Mshahara na posho zake kwa mwezi.
- 11. Kila Mtumishi atakayeomba mkopo atadhaminiwa na mdhamini aliyemdhamini katika ajira yake.
(b)
Mkopo wa Elimu kwa watumishi
Mkopo huu unalenga kuwasaidia watumishi katika kukabiliana na changamoto ya ada kwa ajili ya kulipia gharama za mafunzo katika shule na vyuo mbalimbali.
- Vigezo vitakavyotumiwa na kamati ya Mikopo:-
- 1. Mtumishi atapaswa kujaza fomu maalum ya Watumishi kwa ajili ya kuomba mkopo.
- 2. Mkopo huu utatolewa mara mbili kwa mwaka yaani kulingana na mihula ya shule na vyuo. Kiwango cha juu cha kukopa kitakuwa Tsh.1, 000,000/=.
- 3. Muda wa marejesho wa mkopo huu utakuwa miezi mitatu hadi sita
- 4. Mkopo huu utatolewa kwa riba ya 0.5%
- 5. Utoaji wa mkopo huu utazingatia bakia ya 20% ya mshahara na posho kwa mtumishi.
- 6. Mtumishi atatakiwa kuambatanisha na fomu ya kukubaliwa kujiunga na chuo.